Habari

Kongo kusitishwa mapigano kuanzia Ijumaa

Viongozi wa Afrika wamekubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Ijumaa.

DRC kusitishwa mapigano
Wakilenga kusitisha kabisa mashambulizi ya kundi la waasi la M23. Tamko hilo limetolewa na viongozi wa Kongo, Rwanda, Burundi na Angola, na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, baada ya mkutano wa kilele mjini Luanda uliolenga kutafuta suluhu kwa mgogoro wa mashariki mwa Kongo.

Mbali na kusitisha mapigano taarifa hiyo ilisema kwamba waasi wa M23 lazima waondoke kwenye maeneo yake inayokalia au ikabiliane na vikosi vya jumuiya ya kikanda ya Afrika Mashariki.

Juhudi za kupata tamko kutoka kwa msemaji wa jeshi la M23 hazikufanikiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents