Uncategorized

Korea Kaskazini yakiri kufanya majaribio ya kombora jipya

Korea Kaskazini imesema kuwa imefanyia majaribio silaha yenye kombora kali , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Kim Jong un kugonga mwamba.

Kim Jong Un akihudhuria mafunzo ya kijeshi

Vyombo vya habari vya serikali vilitoa maelezo , lakini wachanganuzi wanansema kuwa jaribio hilo halionekani kuwa lile la kombora la masafa marefu ambalo ni tishio kwa Marekani.

Jaribio jingine kama hilo mnamo mwezi Novemba lilionekana kama hatua ya kuishinikiza Marekani kurudi katika meza ya mazungumzo.

Kumekuwa na hatua chache zilizopigwa tangu mazungumzo ya kinyuklia yaanze msimu wa joto uliopita.

Mnamo mwezi Februari , Donald Trump na Kim Jong Un walikutana katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi kuzungumzia usitihswaji wa umiliki wa silaha za kinyuklia , lakini mazungumzo yalivunjika huku viongozi wote wawili wakiondoka ghafla.

Wiki iliopita bwana Kim alisema kuwa rais Trump alifaa kuwa na tabia nzuri ili ,mazungumzo kuendelea.

Kulingana na chombo cha habari cha Korea KCNA jaribio hilo lilisimamiwa na bwana Kim mwenyewe.

KCNA iliripoti kwamba jaribio hilo lilifanywa katika awamu kadhaa za kulirusha , ambapo wachanganuzi wanaamini huenda silaha hiyo ilijaribiwa kutoka katika ardhi, baharini ama angani.

Bwana Kim alisema kuwa hatua hiyo ilikuwa na uzito mkubwa katika kuimarisha jeshi lake.

Ripoti hiyo ilitoa maelezo machache hivyobasi haijulikani iwapo lilikuwa kombora , lakini wadadisi wanasema kuwa huenda ilikuwa silha ya masafa mafupi.

Mwaka uliopita , kiongozi huyo wa Korea alisema kuwa atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia na kwamba hatofanyia majaribio makombora ya masafa marefu huku uwezo wa Kinyuklia wa Pyonyang ukibainika.

Vitendo vya kinyuklia vilionekana vikiendelea, hatahivyo picha za Setlaiti katika kiwanda kikubwa cha kinyuklia cha taifa hilo wiki ilioipita zilionyesha kulikuwa na vitendo vilivyokuwa vikifanyika-zikidai kwamba huenda Korea kaskazini inatengeneza mionzi kuwa mafuta ya bomu.

Taifa hilo linadai kwamba limetenegeza bomu la kinyuklia ambalo linaweza kuingia katika kichwa cha silaha ya masafa marefu pamoja na kombora ambalo linaweza kufika Marekani,

Mchanganuzi wa Korea Kaskazini Ankit Panda alisema kwamba tangazo hilo la mwisho lilifuatia zoezi la kijeshi lililofanyika kati ya Marekani na Korea kusini na kusema kuwa jaribio hilo lilipanga kulipza kisasi.

Je mazungumzo ya silaha za kinyuklia yamefikia wapi?

Ni hatua chache zilizopigwa tangu mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuvunjika mjini Hanoi.

Marekani ilisema kuwa mazungumzo hayo yalivunjika baada ya Korea Kaskazini kutaka vikwazo vyote kuondolewa ili kuweza kupunguza uwezo wake wa utenegenezaji wa silaha za kinyuklia , lakini Pyongyang imepinga hilo.

Katika matamshi yake ya hivi karibuni , bwana Kim alimtaka Trump kutafuta makubaliano ambayo yatakubaliwa na pande zote mbili lakini pia akazungumzia kuhusu uhusiano wake mzuri na rais Trump.

Naye bwana Trump alijibu kupitia mtandao wake wa Twitter kwa kumsifu bwana Kim na kukubali wazo jingine la mkutano mwengine.

Mapema wiki hii wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani ilitangaza kuwa Stephen Biegun , mjumbe maalum wa Korea Kaskazini alikuwa anaelekea Moscow kwa mikutano na maafisa wa Urusi ili kuzungumzia kuhusu hatua ya mwisho ya kuangamiza silaha za kinyuklia nchini Korea Kaskazini.

Ziara hiyo ilijiri huku kukiwa na uvumi kuhusu mkutano wa Kim Jong Un na Vladmir Putin.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents