FahamuHabari

Korea Kusini yapiga marufuku kuchinja na kuuza nyama ya Mbwa

Moja ya habari kubwa nchini Korea Kusini ambayo imepokelewa tofauti na raia wa nchi hiyo kutokana na utamadini wao ni hii ambapo Bunge la Korea Kusini tayari imepitisha sheria mnamo Januari 9, 2024, ambayo inapiga marufuku uzalishaji, uuzaji na uchinjaji wa nyama ya mbwa, ambayo itaanza kutekelezwa mnamo 2027.

Habari hii imepokelewa tofauti na raia wa nchi hiyo kwa sababu ya kuwa walizoea kuifanya nyama ya Mbwa kama ni Nyama halali kama ilivyo kwa wanyama wengine wanaoliwa/kuchinjwa na nyama zao kuuzwa hadharani.

Sheria hiyo, inayopokea usaidizi kwa kauli moja, inalenga kushughulikia masuala ya haki za wanyama na mabadiliko ya kijamii, huku raia wengi wa Korea Kusini hawatumii tena nyama ya mbwa.

Ukiukaji wa sheria hii utasababisha adhabu, ikiwa ni pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela au faini kubwa, kuonyesha mwelekeo unaokua kuelekea ustawi wa wanyama na kubadilisha mitazamo ya kitamaduni.

Written by @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents