Zimebaki siku 3, Kufungwa kwa Dirisha la Masahihisho ya maombi ya mikopo kwa Wanafunzi 2024/2025
Ni Bodi ya Mikopo Tanzania (Heslb) inapenda kutoa taarifa kwa Waombaji wa Mikopo ya Wanafunzi kwa Mwaka 2024/2025 kuwa baada ya kufanya uhakiki wa maombi yao, imebainiwa baadhi ya maombi hayo yanahitaji kufanyiwa masahihisho ili kuruhusu kuendelea kwa hatua inayofuata.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt. Bill Kiwia amesema ‘Tunapenda kuwataarifu waombaji wote wa Mikopo ya Elimu ya Juu kuwa tunatarajia kufunga dirisha la Masahihisho ya maombi ya Mikopo ifikapo tarehe 21.09.2024 saa 5:59 Usiku.Wote walioomba Mikopo wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kuona iwapo wanahitajika kufanya marekebisho’
Aidha, Maombi mapya hayatapokelewa kwani dirisha la maombi ya mkopo kwani limefungwa rasmi Septemba 14, 2024.