HabariMichezo

Kuiona Yanga huko Rwandwa ni elfu 13

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe amefunguka maandalizi ya timu yake safari kwenda nchini Rwanda kwaajili ya kucheza mchezo wa ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Merreikh ya Sudan ambao watakuwa wapo uwanja wa nyumbani kwa kikanuni.

Lakini baadhi ya taarifa Zinasema Al Merreikh mpaka sasa hawajatangaza bei za viingilio vya mchezo na mashabiki wa Yanga SC wanaenda kwa wingi mpaka sasa kwa mujibu wa msemaji ni mabasi 37,Kamwe anaweka wazi kuwa timu yao kupitia viongozi wao wameshafanya Mawasiliano na Shirikisho la Rwanda pamoja na timu pindani Al Merreikh na wamepewa tayari bei zao za viingilio.

“Tumewasiliana na Shirikisho la Rwanda (FERWAFA) na wapinzani wetu Al Merreikh ya Sudan tayari wametupa bei za viingilio vyote labra niwaibie Siri Mashabiki na wanachama wa Yanga bei ya viingilio vya mchezo katika maeneo ya mzunguko ambavyo ni bei ya chini ni Shillingi elfu 13 za Kitanzania”Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ally Kamwe

Credit by Issaya Dede

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents