BurudaniHabariMichezo

Kuluna walipita na Yanga walivyoenda Lubumbashi

KULUNA WALIWAPITIA YANGA WALIPOENDA LUBUMBASHI

Msanii wa Muziki wa Dance Fabrice Mauzo katika mahojiano na Bongo5 amefunguka mengi yanayoendelea nchini kwake DR Congo ikiwemo taarifa iliyoshtua zaidi Ulimwengu juu ya Vijana zaidi ya 170 waliohukumiwa kifo nchini DR Congo vijana hao maarufu kwa jina la Kuluna.

Ameelezea maoni yake juu ya hilo tukio huku akidai hata klabu ya Yanga yale malalamiko ya baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo walipoenda Lubumbashi kucheza na TP Mazembe walipigwa na kuibiwa na Vijana hao wa Kuluna.

Pia Msanii Fabrice Mauzo mbali na kuachia kibao chake kipya cha ‘NDOA’ anatarajia kuendelea kutoa nyimbo nyingine akiwashirikisha wasanii mbalimbali kutoka Tanzania huku ndoto na kiu Yake kubwa na kuimba nyimbo moja na Msanii Diamond Platnumz.

Kuangalia video kamili tembelea ukurasa wetu wa Youtube Bongo5

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents