Habari

‘Kuna watu hawajachukua kwa miaka 4, na taarifa zao walizojaza hazionyeshi wapo wapi’ (Video)

Hiyo ni kauli imetolewa wiki hii na Gideon Kapange msajili wa Hisa kutoka kampuni ya CSD & Registry Company Limited, Kampuni tanzu ya soko la Hisa la Dar Es Salaam ambayo ndio wasajili na watunzaji wa daftari la wana hisa wa Benki ya Maendeleo.

Amesema benki hiyo ina wanahisa zaidi ya 10,000 na nusu ya hao hawajachukua gawio lao kwa muda mrefu na benki haina taarifa zao.

Gideon amesema wengi wao taarifa ambazo waliziandika hazipatikani na wametangaza katika vyombo mbalimbali vya habari bila mafanikio.

Amesema pesa hizo zaidi ya Tsh Mil. 200 wataendelea kubaki nazo kwa kuwa sheria bado haielezi watu hao wakikosekana pesa hizo zipelekwe wapi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents