Habari

Kundi la kwanza la wakimbizi 51 wa Afghanistan lawasili Uganda

Taarifa kutoka Wizara ya mambo ya nje ya Uganda inasema kundi hilo limewasili leo asubuhi katika uwanja wa kimataifa wa Entebbe kupitia ndege binafsi.

Wizara hiyo imeongeza kuwa kundi hilo linapita tu Uganda na litaelekea Marekani na nchi nyingine, ingawa haijafahamika kundi hilo litakaa Uganda kwa muda gani.

Watu hao walifanyiwa vipimo vya virusi vya korona na watakaa karantini, taarifa hiyo imesema.

Uganda imepokea watu hao kufuatia maombi ya serikali ya Marekani ya kutaka nchi hiyo isaidie kupokea watu wanaokimbia ghasia za Afghanistan tangu kundi la Taliban lishike hatamu juma lililopita.

Wiki iliyopita serikali ya Uganda iliiambia BBC kwamba nchi hiyo inatarajia kupokea wakimbizi 2,000 kutoka Afghaistan kutokana na maombi ya Marekani. Lakini maafisa wa juu wa serikali baadae walisema kwamba mazungumzo bado yanaendelea.

Uganda inawahifadhi wakimbizi zaidi ya milioni 1 kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambao wamekimbia nchi zao kwa sababu ya vita na majanga mengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents