Habari

Kupatwa kwa Jua ilivyotokea baadhi ya maeneo

Kama ilivyotangazwa siku za nyuma kuwa ifikapo tarehe 8 ya mwezi wa nne mwaka 2024 litatokea tukio kubwa Duniani la kupatwa kwa Jua.

Tukio hilo lilitokea kwenye baadhi ya maeneo na hii ni kutokana na mzunguko wa jua lenyewe.

Baadhi ya maeneo ikiwemo Marekani Kaskazini, Canada na Mexico walishuhudia tukio hilo ambalo lilitokea majira ya Saa 7:00 mchana ambapo kwa saa za huku ni Usiku.

Tukio hilo lilichukua muda wa Dakika 4 na sekunde 28 tu na likielezwa ndio limechukua muda mrefu zaidi ya mwaka 2017 ambapo tukio hilo lilichukua dakika 2 na sekunde 42.

Wanasayansi wanasema kupatwa kwa Jua kunaweza kudumu kwa muda wa kuanzia sekunde 30 mpaka dakika 7 na nusu na wanasema mara nyingi kutokana na mzunguko wa jua.

Wamarekani walifurahia sana tukio hilo ambapo kulikuwa mchana  mara kukawa usiku kwa dakika 4 na sekunde 42.

Je mara ya mwisho lini wewe kushuhudia tukio la kupatwa kwa Jua??

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents