Habari

Kuwa Sehemu ya Mabadiliko – Mbio za Baiskeli za Vodacom Twende Butiama 2024

Zuweina Farah (kulia), Mkurugenzi wa Mahusiano Vodacom na Vodacom Tanzania Foundation, akizungumza wakati wa uzinduzi wa msafara wa Vodacom Twende Butiama Mwaka 2024 utakaoanzia jijini Dar es Salaam Septemba 28 na kukamilika Oktoba 14 katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama alikozaliwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wengine kuanzia kushoto ni Gertrude Mongella, Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuki Bgoya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota, na Gabriel Landa, Mwanzilishi wa Twende Butiama wakiwa katika tukio hilo lililofanyika tarehe 1 Agosti, 2024 jijini Dar es Salaam.


Dar es Salaam, Agosti 0
1, 2024 – Tanzania inapoelekeakuadhimisha miaka 25 tangu kufariki kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vodacom Tanzania na Klabu ya Baiskeli yaTwende Butiama wametangaza kufunguliwa rasmi kwa usajiliwa mbio za baiskeli za Twende Butiama Mwaka 2024. Mbiohizo, zitakazofanyika kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 14, zinaadhimisha urithi wa Baba wa Taifa kupitia uendeshajibaiskeli, shughuli za kijamii, na hisani.

Gertrude Mongella, Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa msafara wa Vodacom Twende Butiama Mwaka 2024 zitakazoanzia jijini Dar es Salaam Septemba 28 na kuisha Oktoba 14 katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama alikozaliwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kushoto kwake ni Mkuki Bgoya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota wakiwa katika tukio hilo lililofanyika tarehe 1 Agosti 2024 jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kusaidia jamii kuboresha elimu, afya, na mazingira wakati wa msafara huo utakaochukua siku 14.


Mbio
za Twende Butiama zilianzishwa mwaka 2019 na kikundicha waendesha baiskeli, ili kuadhimisha upendo wa Mwalimu Nyerere wa kuendesha baiskeli na maono yake kimaendeleokatika maeneo matatu muhimu ambayo ni elimu, afya, nautunzaji wa mazingira ambayo yanaweza kuwasaidiaWatanzania kupiga hatua kijamii na kiuchumi.

Tunayofuraha kubwa kufungua rasmi usajili wa Vodacom Twende Butiama Cycling Tour 2024. Mwaka huu hatuadhimishitu kumbukumbu ya Baba wa Taifa bali pia tunalenga kuletamabadiliko yanayodumu kwa muda mrefu. Washirikiwatajumuika katika kampeni kuhusu utunzaji wa mazingira, kuboresha mazingira ya kujifunzia, na kusaidia katikaupatikanaji wa huduma za afya kwa wote kupitia kambi za matibabu. Tunawakaribisha waendesha baiskeli wa ngazi zotekutoka ndani na nje ya Tanzania kujiunga nasi kwenye tukio hilila siku 14 na kufikia zaidi ya Kilomita 1500 katika mikoa 12 nchini,” alisema Gabriel Landa, Mwanzilishi wa mbio za baiskeli za Twende Butiama.

Kwa mwaka wa pili mfululizo Vodacom Tanzania imekuamdhamini mkuu wa mbio hizi na walielezea dhamira yao katikakufikia malengo ya mwaka huu. Mwaka jana, kwa kushirikianana Twende Butiama, walifanikiwa kupanda miti zaidi ya 6000, na kutoa huduma za afya kwa watu zaidi ya 3200 katika wilaya tatu ndani ya mikoa ya Mwanza na Mara. Pia, tukio hiloliliambatana na utoaji wa jumla ya madawati 610 katika shule 13 za msingi. Juhudi hizi zinaendana na malengo ya Vodacom Tanzania ya kuwawezesha watu na kulinda ustawi wa sayariyetu.

“Mwaka huu, tunajivunia kuendelea kuwa sehemu ya jambo hililinalochangia kuleta mabadiliko Chanya kwenye jamii. Mbio za mwaka 2024 zimepanua wigo, kujumuisha mafunzo ya ujuzi wakidijitali na kambi za matibabu zitakazohusisha uchunguzi naelimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza kwenye mikoa 12 nchini. Tunawahimiza waendesha baiskeli wote wa umbalimrefu na mfupi kujisajili na kuungana nasi kufanikisha jambohili. Hii ni pamoja na wadau wengine na wapenda maendeleowalio tayari kushirikiana nasi,” alisema Bi. Zuweina Farah, Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Tanzania Foundation.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents