
- Kocha mpya wa Yanga, Hamdi Miloud mwenye uraia pacha wa Algeria na Ufaransa, ambaye amerithi mikoba ya Sead Ramovic, ameeleza kuwa na mpango wa kuifanya timu hiyo kuwa tishio Ligi Kuu kulingana na ubora wa wachezaji alionao.
.
Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA A, anasisitiza kuwa lengo lake ni kuleta mabadiliko makubwa kwa kutambulisha mfumo wa soka la kuvutia, lenye mashambulizi ya nguvu na ulinzi imara.
.
Mfumo anapenda kuutumia zaidi ni (4-2-3-1), kwa maana ya mabeki wanne, viungo wakabaji wawili, viungo washambuliaji watatu na straika mmoja.
.
Miloud anajipanga kuhakikisha mchezaji mwenye kipaji na anayejituma kuanzia mazoezini hadi katika mechi sambamba na nidhamu yake ndiye atakayekuwa kupata nafasi ya kuiwakilisha timu yake.
.
Mastaa waliokuwa wanapata nafasi mbele ya kocha Ramovic na wale ambao walikuwa wanakaa benchi watakuwa na vita mpya mbele ya Kocha mpya ambaye ameshawaambia mabosi wa klabu hiyo kwamba hajawahi kuishia kwa kukariri katika kupanga kikosi chake
kuangalia video kamili bonyeza link hapa chini: