
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini, Ronaldo hajachora ‘tattoo’ kwenye mwili wake.
Licha ya mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja ambayo Mshambuliji Bora kabisa duniani, Cristiano Ronaldo amekuwa akiyapata pamoja na rekodi mbalimbali anazo endelea kuandika ulimwenguni lakini bado staa huyo ana kitu cha kipekee sana ‘UNIQUE’ ambacho watu wengi wakipata umaarufu hutamani kufanya.<
Mnamo mwaka 2012, Cristiano Ronaldo aliiambia tovuti ya habari ya Italia Diretta sababu za yeye kutokuwa na ‘tattoo’ ni kwa sababu aweze kuchangia Damu yake mara nyingi zaidi.

Kwa mujibu wa National Health Service (NHS) wachangia damu wanapaswa kusubiri miezi minne baada ya kujichora tattoo au kutoboa ngozi kabla ya kuchangia tena.
Ronaldo pia alijisajili kama mchangiaji wa Uroto (bone marrow) uji uji unaopatikana ndani ya mifupa lakini pia alianza kutoa damu yake mara kwa mara baada ya mtoto wa mchezaji mwenzake wa Ureno, Carlos Martins kugundulika kuwa na ugonjwa wa ‘leukaemia’ mwaka 2011.
Imeandikwa na @fumo255