Technology

Kwanini bodi imekubali kumuuzia Elon Musk Twitter ? fahamu zaidi na kiasi anachotoa

Bodi ya Twitter imekubali kumuuzia kampuni hiyo bilionea Elon Musk kwa dola bilioni 44 (£34.5bn) . Bw Musk, ambaye alitoaazma ya kushangaza ya kununua kamouni hiyo wiki mbili zilizopita, alisema Twitter ina “uwezo mkubwa” ambao utafunguliwa.

Pia alitoa pia wito wa msururu wa mabadiliko kuanzia kulegeza masharti ya maudhui yakke ili kuondoa akaunti gushi za mtandao huo wa kijamii.

Awali kamouni hiyo ilipinga dau la Bw Tusk, lakini sasa itawaomba washika dau kupiga kura kuidhinisha mkataba.

Bw Musk ni mtu tajiri zaidi duniani, kulingana na jarida la Forbes , huku akikadiriwa kuwa na utajiri wa tamani ya dola bilioni 273.6,mnyingi kati yake akizipata kutokana na hisa zake katika kampuni ya kutengeneza magari ya umeme Tesla ambayo binafsi anaiendesha. Pia anaongoza kampuni ya safari za anga za mbali SpaceX.

Mwanzoni hadithi ya Twitter na Elon Musk ilikuwa ni kama hadithi ya upendo ambao anayependwa haufurahii.

Elon Musk anaipenda Twitter. Ana ufuasi mkubwa wa watu milioni 83.3 . Hutuma jumbe za Twitter kwa wingi, mara nyingine zenye utata, mara chache huwa ni za ajabu.

SEC ilimpiga marufuku kutuma jumbe za Twitter kuhusu masuala ya Tesla baada ya ujumbe wake mmoja kumaliza bei yake ya hisa yad ola bilioni 14 , na alishitakiwa kwa kutoka kauli ya udhalilishaji ,kufuatia ujumbe wa Twitter alioutuma kuhusu mzamaji wa pangoni ambaye alimuita “pedo guy” (mzamiaji wa pango aliyepotea). Lakini hajawahi kukoma kutuma jumbe za Twitter

Twitter kwa upande mwingine inashauku kidogo sana kumuhusu Elon Musk.

Unaweza kufikiria, kama mtu fulani alikupatia ofa ya dola bilioni 44 kwa ajili ya mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 16 ambaye bado kusema kweli hajafurahia ukuaji wa mshindani wake, anakusaidia – na wanahisa wa Twitter wanaonekana kuelekea kukubaliana na hilo.

Anataka kuona Twitter ” uwezo wake wa ajabu “, anasema – na hata hataki kutengeneza pesa kwa njia ya Twitter . Anazo za kutosha tayari, na bilionea huyu anaweza kuwa na vipaumbele tofauti vingine vya kumpatia pesa.

Twitter ilijibu kwa kujilinda moja kwa moja, kuweka mkakati wa ”kidonge cha sumu” ambacho kilimzuwia mtu yeyote kumiliki zaidi ya 15% ya hisa zake ingawa washirika wa Musk wanafikiri kwamba mkataba sasa umefikiwa.

Labda bodi ya Twitter ilikasirishwa na tangazo la Musk kwamba alitaka kuona zaidi ya “uhuru wa kujieleza” na udhibiti mchache wa Twitter.

Warepublicans wengi , ambao kwa muda mrefu walihisi sera ya udhibiti wa Twitter, unaupendelea wa uhuru wa kujieleza wa maoni yenye mrengo wa kushoto- walishangilia.

Lakini wadhibiti kote duniani wanaungana kukabiliana na mitandao ya kijamii na kuilazimisha kuwajibuka zaidi kwa maudhui yanayotolewa kwenye mitandao hiyo, na kutoza faini kali kwa wasiofuata sheria kuhusu taarifa zinazochochea ghasia, au matusi, au maneno ya chuki.

An illustration of Bitcoin
Je Musk anaweza kutumia Twitter kwa malipo ya motisha katika hali tete, isiyo salama ya sarafu za mtandaoni kama vile Bitcoin?

Tusisahau pesa. Njia kuu ya mfumo wa biashara wa Twitter ni wa misingi ya matagazo ya biashara-na Musk anataka kubadilisha hilo.

Anataka zaidi usajiri wa watu mtandaoni , anadai kile ambacho kinaweza kuonekana kuwa mauzo magumu katika mazingira ambapo mitandao yote mikuu ya kijamii inaweza kuwa huru kukitumia.

Watumiaji wa Twitter wanaweza kuamua kutumia data zao zisitumiwe kwa matumizi ya pesa na wako tayari kulipia hilo-lakini ni suala la kubahatisha.

Anataka sarafu ya mtandaoni kama crypto-currencies. Iwapo atatumia jukwaa la Twitter kwa malipo ya motisha katika utata wa sarafu zisizolindwa kama vile Bitcoin?.

Na halafu kuna Musk mwenyewe. Ni mtu Tajiri zaidi duniani, mjasiriamali sugu ambaye mafanikio yake ni pamoja na makambuni ya PayPal na Tesla. Ni mtu mwenye mvuto – jambo ambalo linaweza kumfanya afanye chochote. Hupenda kujaribu mambo yanayoonekana kuwa ni magumu na kuvunja sheria.

Kuna sababu ni kwanini alikataa kujiunga na bodi ya Twitter baada ya kununua 9.2% ya hisa zake katika mwezi wa januari-hakutaka kubanwa na uwajibikakaji.

Na anajeshi la mashabiki wafuasi wanaomuhusudu- wakati mmoja nilituma ujumbe wa Twitter kuhusu ukweli kwamba, kwasababu ya namna fedha zake zimeundwa(utajiri wake ni wenye misingi ya hisa zaidi kuliko mapato ya pesa, na hamiliki mali) – halipi kodi ya mapato.

Ninawezaje kusema kwamba anaweza kuwa, mwenye akili na tunapaswa kumshukuru yeye, nilijibiwa.

 

Ni mauzo ya kibinafsi, ya kampuni binafsi, na sio ya muungano wa makampuni mawili makubwa, kwa hiyo haiwezekani kuwe na vikwazo vya udhibiti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents