Fahamu

Kwanini jamii ya wakristo hatari kuangamia iwapo mzozo wa Israel na Plaestina utaendelea ? (+ Video)

Chini ya Juma moja , mzozo kati ya Israel na Palestina umeongezeka na kusababisha ghasia chungu nzima. Umewawacha watu 127 wakiwa wamefariki na mamia kujeruhiwa katika mashambulizi ya pande zote mbili.

Ni hali ngumu zaidi katika kipindi cha miaka mitano , na Umoja wa mataifa unahofia kuzuka kwa vita vya kiwango cha juu. Na kati ya mzozo huo , jamii za wachache wanatathmini jinsi mzozo huo ambao haujatatuliwa kwa miaka 70 unahatarisha uwepo wao.

Wakristo wa Palestina waliohamia katika eneo hilo na ambao wanawakilisha asilimia moja ya idadi ya watu katika eneo hilo , wanasema kwamba njia mbadala iliopo ni kuondoka . ”Sisi sio Wakristo tu. Tuko zaidi ya Wapalestina Waarabu na kila kitu kinachofanyika hapa kinatuathiri moja kwa moja” , anasema Bandak Saleh, Mkristo wa Orthodox anayeishi Bethlehemu katika eneo la West Bank alipozungumza na BBC Mundo.

Iwapo mzozo huo hautatatuliwa , hakutakuwa na Wakristo katika ardhi ambayo Yesu alizaliwa, anasema. Wengi wa Wakristo wanaoishi Jerusalem ni Wapalestina.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents