Mwaka 2007, Lionel Messi akiwa mdogo alipiga picha na mtoto kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Camp Nou huko Barcelona kwa picha ya kalenda ya hisani iliyoandaliwa na shirika la UNICEF ambalo ni shirika na kuhuduma Watoto.
Messi alikuwa akimuogesha Lamine Yamal, Picha ya Messi na Yamal iliyosahaulika kwa muda mrefu iliibuka tena baada ya babake Yamal kuiweka kwenye Instagram wiki iliyopita ikiwa na maandishi: “Mwanzo wa hadithi mbili.”
Picha hizo zilichukuliwa na Joan Monfort, ambaye anafanya kazi kama mpiga picha wa kujitegemea wa chombo cha habari cha Associated Press.
Picha hiyo ilitokea baada ya Unicef kucheza mchezo wa bahati nasibu katika mji wa Mataró ambako familia ya Lamine iliishi, alisema.
“Walijiandikisha kwa bahati nasibu ili picha yao ipigwe huko Camp Nou wakiwa na mchezaji wa Barca. Na walishinda bahati nasibu,” Bw Monfort aliambia Associated Press.
Picha hiyo haikuwa ya moja kwa moja, mpiga picha alisema.”Messi ni mvulana anayevutia, ana haya,” alisema.
“Alikuwa akitoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo na ghafla akajikuta kwenye chumba kingine cha kubadilishia nguo akiwa na beseni la plastiki lililojaa maji na mtoto ndani yake. Ilikuwa ngumu.
Hakujua hata jinsi ya kumshika mwanzoni
Kama Messi, Yamal alienda kuichezea Barcelona, ambapo alikua mwanzilishi na mfungaji mabao mdogo zaidi katika klabu hiyo, na pia mfungaji mdogo zaidi wa mabao katika ligi ya Uhispania.
Bw Monfort alisema ni wakati tu picha hiyo ilipoanza kusambazwa mitandaoni wiki jana ndipo alipogundua kuwa mtoto huyo alikuwa Yamal.
https://youtu.be/wIeIhoyzLwo?si=HpA_KJVZVUaSGqs9