Kwanini Trump anakitaka kinu kikubwa zaidi cha nyuklia Ulaya huko Ukraine?

Wazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu maslahi ya Marekani kuchukua udhibiti wa kituo kikubwa cha nishati ya nyuklia cha Ukraine lina changamoto kubwa kwa mtu maarufu kwa sanaa ya kufanya mikataba: itachukua miaka mingi kabla ya kuwa na matumaini yoyote ya kurejesha faida kutoka kwa uwekezaji huo.
Kiwanda hicho kikubwa cha nyuklia, ambacho Urusi imekikalia tangu mwanzo wa uvamizi wake wa 2022, kimejaa matatizo makubwa.
Vinu vyake sita vya nyuklia zake vimezimwa, kuna uharibifu wa bomba kuu la kusambaza maji ya baridi na hakuna anayeweza kusema hali ya vifaa vyake vingine vikoje.
Katika mazungumzo yao kwa simu siku ya Jumatano wiki hii, Trump alimwambia Zelensky kwamba Marekani inaweza kusaidia kuendesha, na pengine kumiliki, mitambo ya nishati ya nyuklia ya Ukraine, kulingana na taarifa kutoka kwa utawala wa rais wa Marekani.
Akizungumza baadaye, Zelensky alisema kuwa walijadili kiwanda cha Zaporizhzhia pekee katika simu hiyo: “Rais aliniuliza kama kuna makubaliano kwamba Marekani ingeweza kukarabati kiwanda hiki, na nilimjibu ndiyo, ikiwa tutaweza kukiimarisha na kuwekeza fedha.”
Vyanzo viwili vya sekta ya viwanda vya Ukraine vimesema pendekezo hili linaweza kuwa mfano wa Marekani kujaribu mawazo mbalimbali ili kuona kile kinachowezekana, huku Trump akitafuta kufikia mkataba wa amani wa kudumu utakaomaliza haraka vita kati ya Urusi na Ukraine.
Moja ya vyanzo hivyo walisema wazo hili pia linatoa shinikizo kwa Urusi kwa kupendekeza mpango ambao wangekubali kukabidhi kiwanda hicho.
Wamarekani walikuwa wakichochea hali hiyo kwa kutumia neno “umiliki”, kilisema chanzo hicho.
Zelensky amesema itachukua miaka miwili na nusu kurejesha kiwanda hicho, ambacho ni kikubwa zaidi cha aina hiyo barani Ulaya.
Msemaji mmoja wa zamani wa serikali ya Ukraine alisema “yote yanawezekana na Wamarekani, lakini hili ni jambo lisilo rahisi.
“Wamarekani wangeweza kumiliki – lakini kwa misingi gani? Kinamilikiwa na Ukraine. Sawa, hebu tukikabidhi kwa Marekani – lakini kwa misingi gani? Watakinunua? Watakichukua kama sehemu ya makubaliano? Maswali mengi.”
Marekani anajua nishati zzote za Ukraine ni faida kubwa kwakwe. Na kwakuwa Ukraine yuko matatizoni, anatumia fursa hiyo kutengeneza maslahi ya Marekani kwenye mzozoz huo wa Ukraine.
Kiwanda hicho ni kama ‘sanduku bila mitambo’

CHANZO CHA PICHA,BBC/KOSTAS KALLERGI
Oleksandr Kharchenko, mchambuzi wa nishati kutoka Kyiv, akizungumza na Reuters alisema urejeshaji wa kiwanda hicho kwenye gridi ya umeme ya Ukraine – kama ambavyo Kyiv inavyodai – itakuwa “mabadiliko makubwa” katika uzalishaji wa nishati si tu kwa Ukraine bali pia kwa Ulaya ya Mashariki na Kati.
Kituo hicho kilitoa asilimia 20 ya uzalishaji wa umeme wa Ukraine kabla ya vita. Ukraine ilianza kuuza umeme kwa kiasi kikubwa kwa Umoja wa Ulaya kabla ya uvamizi, lakini iliishia kuacha baada ya Urusi kuharibu miundombinu yake kwa makombora na ndege zisizo na rubani.
Kwanini kituo cha Zaporizhia kinashambuliwa?

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) limeeleza mara kwa mara wasiwasi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya kituo cha Zaporizhia, kinu kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, na kupendekeza kuanzishwa kwa eneo la usalama wa nyuklia kukizunguka.
Kulipua kinu cha nyuklia kumefanywa kama “mchezo wa kuigiza”, Olli Heinonen, naibu mkurugenzi mkuu wa zamani wa IAEA, aliiambia BBC.
Hata hivyo, alifafanua kuwa kombora moja haiwezekani kusababisha uharibifu kwenye kinu chenyewe, ambacho kinalindwa kwa kujengewa saruji na chuma umbali wa mita kadhaa.
Hatari, ni kwamba mlipuko huo wa mabomu ungekata umeme kwa mfumo wa kupoeza, ambayo ingemaanisha kinu au mafuta yaliyotumiwa yangepata moto sana, na kusababisha mafuta kuyeyuka na kutolewa kwa mionzi.
Zaidi ni kwamba wafanyakazi “wanaweza kufanya makosa” kutokana na shinikizo lao, ikiwa wana uwezo wa kuuendesha.
“Ni mchezo hatari na lazima usitishwe,” Heinonen aliongeza.
“Habari kutoka kwa timu yetu zinatia wasiwasi sana,” alisema Rafael Grossi, mkuu wa IAEA, ambaye wafanyakazi wake walisema kumekuwa na uharibifu wa baadhi ya majengo, mifumo na vifaa kwenye kiwanda hicho.
“Kumekuwa na milipuko kwenye eneo la kinu hiki kikubwa cha nguvu za nyuklia, jambo ambalo halikubaliki kabisa.
Yeyote aliye nyuma ya hili lazima aache mara moja. Kama nilivyosema mara nyingi, wanacheza na moto,” aliongeza.
Jinsi mashambulizi ya nyuklia yanavyotokea
Msingi wa uwezekano wa makosa ni mifumo ya tahadhari ya mapema iliyowekwa wakati wa Vita Baridi.
Badala ya kungoja makombora ya nyuklia kulenga shabaha yao – ambayo, kwa kawaida, itatoa uthibitisho halisi wa shambulio – haya yanalenga kuyagundua mapema, ili kulipiza kisasi kuweze kurushwa kabla ya silaha zao wenyewe kuharibiwa.
Ili kufanya hivyo, unahitaji data.
Bila Wamarekani wengi kujua , Marekani kwa sasa ina idadi ya satelaiti zinazoitazama kimyakimya wakati wote, zikiwemo nne zinazofanya kazi kutoka maili 22,000 (kilomita 35,400) juu ya Dunia.
Ziko katika “obiti ya geosynchronous” – iko katika sehemu maalum ambapo hazibadilishi kamwe nafasi inayohusiana na sayari wanayozunguka.
Hii inamaanisha kuwa zina mwonekano wa karibu zaidi au mdogo wa eneo moja, kwa hivyo zinaweza kugundua uzinduzi wa tishio lolote la nyuklia, siku saba kwa wiki, saa 24 kwa siku.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Kile ambacho satelaiti haziwezi kufanya ni kufuatilia mkondo wa kombora linaposafiri.
Kwa hili, Marekani pia ina mamia ya vituo vya rada, ambavyo vinaweza kuamua nafasi na kasi yao, na kuhesabu mwelekeo wa silaha kama hizo.
Mara tu kunapokuwa na dalili za kutosha kwamba shambulio linaendelea, rais anafahamishwa.
“Kwa hivyo labda kama dakika tano hadi 10 baada ya kurusha makombora, rais atapata habari,” Perry anasema. Wana kazi isiyoweza kuepukika ya kuamua ikiwa watajibu shambulio.
“Ni mfumo mgumu sana na unafanya kazi karibu kila wakati,” anasema Perry. “Lakini tunazungumza juu ya uwezekano mdogo, wa tukio kenye matokeo ya juu.” Inahitaji kutokea mara moja tu.