Lady Jay Dee
Lady Jaydee atarajia ‘kuamka tena’ hivi karibuni

Lady anatarajia kuamka tena.
Muimbaji huyo mkongwe ambaye yuko kimya kwa miezi kadhaa sasa, anatarajia kuuvunja kwa mradi mpya alioupa jina la ‘Naamka Tena.’
Kupitia Instagram, Jide ameshare video inayomuonesha mchoraji maarufu wa vibonzo, Masoud Kipanya akichora na kuandika kwenye tablet kuwa ‘30 Days To Go.’
Hivi karibuni Jide alikuwa nchini Kenya ambako inavyoonekana alirekodi ngoma kadhaa.
Amekuwa kimya tangu aachie wimbo wake Give Me Love aliowashirikisha Uhuru na Mazet wa Afrika Kusini.