Michezo
Lakred atua kambini Misri
Mlinda Mlango wa klabu ya Simba Raia wa Morocco Ayoub Lakred amewasili katika Kambi ya Klabu ya Simba iliyopo nchini Misri inayojiandaa na msimu mpya 2024/2025.
Lakred anatazamiwa kuchukua nafasi ya Aishi Manula anaetajwa kutimkia Klabu ya Matajiri wa Chamanzi Azam FC.
Ayoub Lakred hakuongozana na Msafara wa Simba uliotoka na kikosi cha Simba Jijini Dar es Salaam.