Habari

LATRA yatoa vibali 150 kwa mabasi kubeba abiria wa Mbezi Luis, Kimara

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo, amewatangazia wasafirishaji wa mabasi ya mjini (daladala) wa Jiji la Dar es Salaam kwamba LATRA inatoa vibali 150 kwa mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 26 na kuendelea, ili kutoa huduma kuanzia Mbezi Luis kwenda Posta, Mnazi mmoja, Muhimbili na Makumbusho.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kuharibika kwa miundombinu ya mabasi ya mwendokasi kutokana na maandamano yaliyosababisha changamoto katika usafiri wa jiji.

Akiongea na waandishi wa habari, CPA Suluo alisema anawatangazia wasafirishaji wa Jiji la Dar es Salaam wa mabasi ya mjini (daladala) kwamba wanatoa vibali kwa wenye mabasi ya kubeba abiria 26 na kuendelea. Walete maombi ya kutoa huduma kuanzia Mbezi Luis kwenda Posta, Mnazi mmoja, Muhimbili na Makumbusho.

“Tuna nafasi 150, na atakayewahi atampa nafasi ya mwanzo. Hii inatokana na changamoto za usafiri wa mabasi ya mwendokasi kwenda Kimara, na vibali hivi vitatolewa kwa kipindi cha miezi mitatu. Tunaamini kwamba wenzetu wa DART watakuwa wamerekebisha miundombinu kufikia wakati huo.” amesema

CPA Suluo pia aliongeza kuwa njia ya Mbagala tayari imetolewa kwa mwekezaji wa Mofat, kwani miundombinu ya eneo hilo haijaathirika sana. Mara marekebisho yatakapokamilika, Mofat atarudi kutoa huduma ya mabasi kwenye eneo hilo.

Taarifa hii inalenga kurejesha ufanisi wa usafiri wa abiria, kuhakikisha huduma inapatikana kwa muda na kupunguza usumbufu uliosababishwa na miundombinu iliyoharibika.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents