Fahamu

Lema: Kumekuwepo na matukio mengi ya hatari nchini,utafiti ufanyike

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kuwa inabidi ufanyike utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, kufuatia uwepo wa matukio mengi nchini ya watu kujiua, watoto kuua wazazi wao ama wazazi kuua watoto wao.

Rai hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, hii leo Januari 14, 2022.

“Kumekuwepo na matukio mengi ya hatari nchini, watu kujinyonga, watoto kuua wazazi, wazazi kuua watoto pia na ulevi wa kupindukia, kuna hitajika utafiti wa haraka wa afya ya akili za watu, ugumu wa maisha na kupoteza matumaini kumeongeza msongo wa mawazo na uchungu, ni hatari sana, “– ameandika Lema

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents