Habari
Leo ni Siku ndefu kwa Makonda

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda leo, Jumatatu Aprili 08, 2024 anatarajiwa kukabidhiwa rasmi ofisi hiyo na mtangulizi wake John Mongela ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara.

Hafla ya makabidhiano hayo inatarajia kufanyika kwenye viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia saa 03:00 asubuhi ambapo viongozi mbalimbali kutoka taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali, vyama vya Siasa, Wadau wa Maendeleo na Wananchi kwa ujumla tukio la makabidhiano.

Ikumbukwe kuwa Paul Makonda ambaye ameteuliwa na kuapishwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni awali alikuwa katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa.
Imeandikwa na Mbanga B.






