LEONBET kumwaga fedha kwa watakao bashiri kwa usahihi matokeo ya Trump dhidi ya Kamala
Wakati joto la uchaguzi mkuu wa Rais wa Marekani uliopangwa kufanyika Novemba 5, 2024 likipanda, kampuni nyota ya michezo ya kubashiri nchini, LEONBET imetangaza kuwapa fedha watakaobashiri kiusahihi matokeo ya wagombea, Donald Trump na Kamala Harris.
Meneja Mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana alisema kuwa wameamua kupanua wigo wa kubashiri kwa wafuatiliaji wa siasa ili na wao waweze kufaidika kupitia ubashiri wao.
Maligana alisema kuwa hii ni nafasi yao ya kipekee ya kutumia maarifa yako kushinda pesa kupitia uchaguzi wa Marekani ambao unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kwa wagombea hao wawili.
“Cha kuvutia zaidi, sasa unaweza kubeti matokeo haya kupitia LEONBET, kampuni mpya ya kubashiri nchini Tanzania iliyokuja na nguvu kubwa, odds za kibabe, na malipo fasta,” alisema Maligana.
LEONBET inachukua Soko la Kubeti Tanzania kwa Kishindo
Kwa mujibu wa Maligana, kwa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya kubashiri, LEONBET imefanikiwa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja wake ulimwenguni kote.
“Sasa, kampuni hii yenye uzoefu mkubwa imekuja Tanzania na inaleta mabadiliko makubwa kwenye soko la kubeti mtandaoni.
Kwa watumiaji wa Tanzania, LEONBET inaleta mambo mengi ya kuvutia kama Odds Kubwa – Beti zako zinaweza kukupatia ushindi mkubwa zaidi na pili malipo ya haraka ambayo uwawezesha washindi kupata malipo papo hapo,” alisema.
Pia alisema kuwa kampuni yao imepanua wigo wa kubashiri (Masoko Mengi ya KubetI) ambayo inawapa fursa wapenda michezo, siasa, au burudani na vile vile kuwapa nafasi ya FREEBET hadi kufikia Sh8, 000 kwa wateja wapya.
“Unapojisajili leo, unapewa FREEBET hadi Sh8, 000 kwenye mwezi wako wa kwanza. Hii ni nafasi yako ya kuanza bila ya kuwekeza pesa zako mwenyewe na kuongeza nafasi yako ya kushinda.” Alisisitiza.
Alisema kuwa ili kuwapa wateja wao huduma bora zaidi, wameamua kuwa hewani kwa wateja wao kwa masaa 24 katika wiki (24/7) na kuwa na michezo ya mingi mbalimbali.
“Kwa wateja wa LEONBET, huduma ya wateja inapatikana masaa 24 siku saba (7) wiki ili kuhakikisha unapata msaada unaohitaji kila wakati. Unaweza pia kufurahia michezo mingi ya kubashiri – iwe ni mpira wa miguu, michezo ya kasino, au matukio makubwa kama uchaguzi wa Marekani,” alisema Maligana.