Michezo

Ley Matampi huyooo

Kikosi cha wachezaji 22 cha Coastal Union na benchi lote la ufundi, alfajiri ya leo Jumatano kimeanza safari kuifuata AS Bravo ya Angola  huku kipa namba moja na timu hiyo, Ley Matampi akijumuishwa.

Coastal Union ambayo inaiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Jumamosi ya wiki hii inatarajiwa kupambana na Waangola hao katika mchezo wa hatua ya awali utakaofanyika kwenye Uwanja wa Tundavala uliopo Lubando nchini humo.

Akizungumza, Kocha Mkuu wa Coastal Union, David Ouma, “Ni vizuri tunaanzia ugenini, tunaenda kutumia vyema mchezo huo kwa kuwaheshimu wapinzani, lengo ni kwenda kupata matokeo mazuri ili kuja kumaliza mchezo nyumbani na hatimaye kutinga hatua inayofuata.”

“Matampi yupo pamoja na timu na ameanza mazoezi ni miongoni mwa wachezaji watakaosafari na timu,” alisema kocha huyo raia wa Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents