Habari

Lifti yaporomoka Millenium Tower kutoka ghorofa ya 10 (+Video)

Lifti iliyopo katika jengo la ghorofa la Millenium (Millenium Tower) Makumbusho, Dar es Salaam, imeporomoka na kujeruhi watu kadhaa waliokuwa wakiitumia.

Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Patrick Mohammed amesema, chanzo cha lifti hiyo kuporomoka ni kuzidisha idadi ya watu tofauti na uwezo wake ambapo wakati tukio hilo linatokea ilibeba zaidi ya watu 10.

Lifti hiyo imeporomoka kutoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Credit by TBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents