HabariMichezo

Ligi kuu Ufaransa kinara kadi nyekundu, msimu huu tu tayari Ligue 1 kadi nyekundu 34 na Ligue 2 kadi 45

Mpaka sasa ikiwa ligi mbalimbali zipo mwanzoni tu mwa msimu, kuna matukio mengi sana ambayo tayari yameshatokea hasa kwenye upande wa adhabu za kutolewa kadi nyekundu na kadi za njano.

Zifuatazo ni Idadi ya kadi nyekundu msimu huu katika ligi tano bora Ulaya na duniani.

Katika ligi ya Ufaransa Ligue 1 na Ligue 2 tumeziweke zote kulingana na namna kadi nyekundu zilivyotolewa msimu huu.

🏴 Ligi Kuu: Kadi 4 nyekundu 🔴

🇩🇪 Bundesliga: Kadi 12 nyekundu 🔴

🇮🇹 Serie A: Kadi nyekundu 🔴 15

🇪🇦 Liga: Kadi nyekundu 🔴 20

🇫🇷 Ligue 1: kadi 34 nyekundu 🔴

🇫🇷 Ligue 2: Kadi 45 nyekundu 🔴

Waamuzi wa Ufaransa tangu mwanzo wa msimu huu ndio wanaongoza kutoa kadi nyekundu zaidi licha ya kuonekana ni moja ya ligi isiyokuwa na mvuto kati ya ligi bora tano duniani.

Kama imefanikiwa kufuatilia ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1 unahisi kwanini waamuzi wanaongoza kutoa kadi nyekundu zaidi?? #Bongo5Updates.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents