Lil Baby akamatwa na Bangi jijini Paris.

Rapa wa Marekani ambae hivi karibuni amenyakuwa tuzo ya BETAwards 2021 katika kipengele cha Best Male Hip-Hop Artist, Lil Baby amekamatwa na polisi wa Ufaransa jijini Paris kulingana na ripoti za TMZ.

Lil Baby yupo jijini Paris kwa ajili ya kuhudhuria Fashion week ambapo alihudhuria onyesho la Balenciaga na akionekana akiingia na mcheza mpira wa Kikapu, James Harden siku ya Alhamisi, Julai 8.

Kulingana na TMZ, rapa huyo alikuwa na Harden patoja na washkaji zake wengine kadhaa walipokamtwa na polisi mnamo Alhamisi.

Ripoti inasema gari alilokuwa akilitumia Lil baby pamoja na wenzake Lilisimamishwa na maafisa na walisikia harufu ya bangi.

Lil Baby alionekana amefungwa pingu akiwa ameketi nyuma ya gari la polisi. Inasemekana alikuwa kati ya watu watatu waliokamatwa kwa shtaka linalohusiana na bangi na inadaiwa kuwa walikuwa na kiasi cha Gramu ishirini za bangi zilizokamatwa.

Vyanzo vinasema Harden hakuvunja sheria yoyote na aliruhusiwa kwenda.

Imeandikwa na Raheem Rajuu.

Related Articles

Back to top button