Linda mali zako ukiwa umebima kupitia benki ya NMB
Benki ya NMB imekuja na bima ya mali ambayo ni maalum kwa ajili ya kulinda mali zako dhidi ya majanga
yatakayotokea ikiwa ni pamoja na jengo na vitu vya ndani ikiwemo samani.
Bima hii inamkinga mteja dhidi ya majanga yatokanayo na moto,radi, tetemeko la ardhi, mlipuko wa Volkano ,
mafuriko, maandamano na migomo yasiyo ya kisiasa, kupasuka au kufurika kwa tanki la maji, bomba au vifaa
vyake.
Aidha, wizi wa kutumia nguvu za kuingia kwenye jengo na kuiba, madhara kwa majengo kutokana na chombo cha moto au wanyama wasiomilikiwa na mwenye bima.
Kwa upande wa viwango vya bima, vinatolewa kulingana na thamani iliyowekwa katika bima, inategemea na
gharama elekezi inayotolewa na mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA).
Mfano;
Thamani ya nyumba(Tshs) Tshs. 100,000,000
Agizo la kiwango(%) cha chini 2018 ni 0.15 0.15
Kiwango bila VAT Tshs. 150,000
Pamoja na VAT 18%(Tshs) Tshs. 27,000
Kiwango(Pamoja na VAT) Tshs. 177,000
Unachohitaji;
Umiliki na Kitambulisho halali
Fomu ya gharama na viwango
Orodha ya vitu na gharama zake
Thamani ya mali
Janga litakapotokea, toa taarifa za madai katika tawi lolote la NMB karibu yako piga simu namba 0800 002 002 bure!
Pia, ambatana na ripoti ya polisi katika masuala ya wizi(loss report) au ripoti ya jeshi la kuzima moto na gharama za marejesho/marekebisho.
Umebima-SiNgumuKihivyo!