Michezo

Lionel Messi amevunja rekodi ya wachezaji hawa, na kuwa mchezaji wa kwanza katika ligi 5 bora barani ulaya, kufikisha magoli 400 katika ligi moja

Mchezaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye pia ndio kapteni wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina amefanikiwa kuvunja rekodi ya wachezaji mbalimbali barani Ulaya.

Messi ambaye anaitumikia Barcelona msimu wa 14 hadi hivi sasa amefanikiwa kuvunja rekodi ya kufikisha magoli 400 katika ligi 5 bora barani ulaya ambazo ni Ligi kuu nchini Uingereza PL, Ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, Ligi kuu nchini Ujerumani, Bundasliga, Ligi kuu nchini Italia Seria A na Ligi kuu nchini Uhispania Laliga kwa kufikisha magoli hayo 400.

Messi akiwa Barcelona amefanikiwa kucheza michezo 435, rekodi ambayo amempita mchezaji kutoka Nchi Ujerumani Gerd Müller
aliyeitumikia Bayern Munich ambaye alifikisha magoli 365 akifuatiwa na Mreno anayeitumikia Juventus lakini magoli haya aliyapachika akiwa La liga Cristiano Ronaldo ambaye alifunga magoli 311.

Katika ligi kuu nchini Uingereza anayeongoza kufunga magoli mengi ni Alan Shearer mwenye magoli 260, Ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1 anayeongoza ni André-Pierre Gignac ambaye alikuwa na magoli 103, Ligi kuu nchini Italia Seria A anayeongoza ni Silvio Piola, mwenye magoli 274 na ligi kuu nchi Ujerumani ni Gerd Müller mwenye magoli 365 na La liga ndio Messi mwenye magoli 400.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents