HabariSiasa

Lissu afafanua “NO REFORM NO ELECTION”, Siyo msimamo wangu

“Tunaposema bila mabadiliko hakuna uchaguzi tuna maana gani? Tuna maaana kwamba kusipokuwa na mabadiliko yanayohitajika ya mfumo wa uchaguzi, tutafanya kila tunaloweza, kwa nguvu tulizonazo kuhakikisha kwamba uchaguzi mkuu haufanyiki mwaka huu, hatuzungumzii kususia uchaguzi, hatutasusia, tutaenda kuwaambia Watanzania, na tutaiambia jumuiya ya kimataifa, na tutawaambia walimwengu kwamba kama CCM na serikali yake haipo tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi huru na za haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa, ndiyo maana ya ‘No Reform No Election’ bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Ninataka niwe wazi hapa, huu siyo uamuzi wa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu, huu ni msimamo wa CHADEMA kama ulivyowekwa na vikao vyake vya juu vya kikatiba: Kamati Kuu, Baraza Kuu, Mkutano Mkuu wa Taifa” – Lissu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam siku ya Jumatano Februari 12, 2025.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents