HabariMichezo

Lonel Messi anukia Saudi Arabia

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari nchini Hispania, Gerard Romero amedai kuwa mshambuliaji wa Paris Saint Germain, Lionel Messi amegoma kuongeza mkataba wa kubakia kwenye timu hiyo huku akihusishwa na timu ya Al Hilal kutoka Saudi Arabia.

Messi amejiunga na PSG mwaka 2021, nakufunga jumla ya magoli 24 assist 28 kwenye michezo 54 aliyoitumikia miamba hiyo ya soka Ufaransa.

Mkataba wa Lionel Messi na PSG unatarajia kufikia tamati 2023, na alisema angeongeza mkataba baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Tangu Cristiano Ronaldo kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia kumekuwa na tetesi kwa Klabu ya Al-Hilal kumtaka Lionel Messi huku wakiweka kitita cha fedha za kimarekani dola milioni 350.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button