Burudani

Lorenzo ni msanii mpya ya BongoFleva wakuangaliwa zaidi mwaka 2019 (Video)

Kila mwanzoni mwa mwaka mpya tumekuwa na desturi ya kutaja orodha ya wasanii wapya wenye uwezo mkubwa wa kuwaangalia zaidi kwenye muziki wa BongoFleva katika mwaka husika, ambapo mwaka 2019 tumeanza kwa kumuangalia zaidi rapa , Lorenzo.

Miaka iliyopita tumekuwa tukitoa orodha ya wasanii 10 wa kuangaliwa zaidi katika mwaka husika, lakini mwaka 2019 tunatoa orodha ya msanii mmoja mmoja wakuangaliwa zaidi ili kila mmoja apate kuelezewa zaidi kuhusu ukee, pamoja na kazi ambazo ameshazifanya.

Lengo la kuwataja ni kuwashawishi wadau wa vyombo vya habari nchini kuwapa nafasi ya kipekee msanii husika kwakuwa ana potential ya kuja kuwa wasanii wakubwa baadaye.

Lorenzo aka Uwezo ni msanii mpya kwenye tasnia ya muziki wa hip hop mwenye uwezo mkubwa wa kuandika na kuchana kwa style tofauti tofauti. Pia ni mtayarishaji wa muziki kutoka studio za Sinza Music yenye makazi yake, Sinza Mapambano jijini Dar es salaam.

Rapa huyo ambaye alizaliwa Tanzania na kukulia nchini, Botswana, ameshatoa ngoma nyingi pamoja na video ambazo hazikupokelewa vizuri na mashabiki wa muziki.

“Nimekulia Botswana, nimesomea huko huko na nimerudi Tanzania baada ya mama yangu kuugua na kansa ya titi, baba yangu alikuwa tayari ameshafariki toka 2003 na ugonjwa wa UKIMWI. Pia mama yangu alikuwa na kansa pamoja HIV kwahiyo baada ya kuja Tanzania hakuchukua muda mrefu akafariki,” alisema Lorenzo.

Aliongeza, “Kwa kuwa Botswana nilikuwa nasomea Sound Engineering na sikumaliza baada ya wazazi wangu kufariki sikuweza kurudi tena Botswana, nikaamua nibaki hapa kwaajili ya kupambana na maisha ya muziki. Basi nikaamua nifanye muziki kwa kuwa naamini ina uwezo mkubwa, naomba mashabiki na wadau wa muziki wanipe nafasi ya kunisikiliza kwa sababu ni kitu tofauti kabisa kwenye muziki ninaoufanya,”

Kwa sasa rapa huyo ameshafanya kolabo na wasanii kadhaa wa muziki nchini Tanzania akiwemo, Billnass, Godzilla na wengine wengi, lakini kolabo ya wimbo ‘Hello’ aliyofanya na Mesen Selekta ndio wimbo wake uliofanya vizuri zaidi.

Lorenzo ni mwandishi mzuri, na ana uwezo wa kuchana na kuimba.

Katika kazi zake ambazo tayari ameziachia kupitia chaneti yake ya YouTube ameonyesha uwezo mkubwa katika ngoma zake. Kwa mfano wimbo ‘No Pressure’ aliuachia Sep 17, 2018 haukupaswa kuwa na views 1220 mpaka sasa kutokana uwezo mkubwa alioutumia kwenye uandishi, message ya wimbo pamoja na beat.

Katika wimbo ‘Love Me Harder’ ndani ya Freestyle Zone ya mwaka 2013, Lorenzo alionyesha uwezo wake mkubwa wa kuimba. Ingawa alitumia kingereza lugha ambayo sio rafiki sana kwa watanzania wengi lakini kipimo cha uwezo wake wajuu kinabaki palepale, kwani waungana wasema muziki hauna lugha hata EFM wanamsemo ‘muziki unaongea’.

Lorenzo ni mtajarishaji wa muziki.

Huyu jamaa ni full mwanamuziki, kwani ana uwezo kuandaa beat, na kupigia vifaa mbalimbali ya muziki hata ngoma zake nyingi ameziandaa wenyewe. Huyu ni producer mkuu wa studio za Sinza Music na alisema lengo la kuwa na studio ni kutaka kupata muda mwingi wa kuandaa muziki wake.

“Msanii ni studio, mimi maisha yangu ni muziki, naamka studio na lala studio, kwa maana hiyo muda wangu mwingi ni studio ndio maana nikaona wakati naanza safari yangu ya muziki lazima niwe na studio ya uhakika ambayo kama namwitaji producer yeyote naweza nikamuomba kwaajili ya kazi, tofauti na kwenda kwenye studio za watu ambazo bila shaka utakuta kunataratibu zao,”

Jambo linalovunja mioyo ya wasanii wengi wachanga ni hawapati ushirikiano kutoka kwa wakubwa wao wenye uzoefu na sanaa. Nahisi ni woga wa kupitwa na chipukizi umetawala kwenye vichwa vya mastaa wetu.

Jambo hilo linakwamisha maendeleo ya sanaa yetu kwa sababu ili tusonge mbele ni lazima kuwe na wasanii wengi wanaochuana vikali kwenye tasnia ya muziki.

Je Lorenzo anasemaje kuhusu ujio wake mwaka 2019.

“Mwaka huu kwangu nataka uwe tofauti kabisa, nina kazi nyingi sana ambazo nimeziandaa, hakuna msanii bila shabiki, binafsi anaona kabisa muziki yangu una kitu ndani yake ndio maana mwaka huu nikaanza kwanza kuzungumza na Watanzania, wadau wa muziki, wasanii wenzangu, naombeni nafasi ya kuonyesha nilichonacho. Kwa sasa muziki una ushindani mkubwa sana, naamini wenye vipaji na muziki nzuri tunanafasi kwasababu muziki nzuri unanguvu sana. Karibuni sana kwenye mitandao yangu ya kijamii naamini ukaribu wenu kwangu utanijenga kwa sababu napokea ushauri,”

Tunahitaji kina Diamond na Alikiba wengine wengi ili tasnia ya burudani ichangamke zaidi ya ilivyo sasa. Mtaani kuna vipaji lukuki lakini nafasi za kuonyesha uwezo wao hazipatikani kirahisi. Na sisi Watanzania ndio wenye maamuzi na uwezo kwenye hili, tuchukue hatua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents