
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais Samia kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, anayepatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Samia na kwamba anafuatilia hali ya Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.
Kwa upande wake mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa, aamemshukuru Rais Samia kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia, huku mtoto wake Fredy Lowassa akiwashukuru Watanzania kwa maombi yao.