
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Klabu ya Inter Milan, Beppe Marotta amesema kuwa Romelu Lukaku atarejea Chelsea mwishoni mwa msimu, bila kujali jinsi miezi ya mwisho ya mkopo wake na timu hiyo itakavyokuwa.
Lukaku alirejea San Siro msimu uliopita kwa mkopo wa muda mrefu, ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya mchezaji huyo kujiunga na Chelsea kutoka Inter kwa ada iliyovunja rekodi ya klabu.
Mshambulizi huyo alikuwa na wakati mgumu sana Stamford Bridge kabla ya kurudi tena Italy ambako anaimarisha kiwango chake huku akiwa amefunga jumla ya magoli matano licha ya kuandamwa na majeraha.
Imeandikwa na @fumo255