Siasa

Lusinde: Kuna watu wanamsema vibaya hayati Magufuli na sisi tupo, hilo jambo halivumiliki washike adabu (+ Video)

Amani na utulivu haviwezi kuwepo kama tuna baadhi ya wabunge na watanzania wanamsema vibaya Hayati Rais Magufuli. Leo najitoa mhanga, haiwezekani tuwe na viongozi wanaojaribu kupinga mambo mazuri aliyoyafanya Magufuli, hatuwezi kuwavumilia”

“Hawahawa wanaomsema vibaya leo Magufuli, watamsema vibaya Rais Samia. Kuna wanofikiri labda Rais Samia alikuwa benchi akaingia kucheza, hapana. Rais Samia alikuwa anacheza pamoja na Magufuli na aliyemtaja Samia ni Magufuli mwenyewe na alijua akiondoka yupo Samia”

“Tunataka watu wamheshimu Magufuli, huwezi kuondoa Legacy yake kwa nchi hii na Afrika. Kuna Mbunge gani hakutetewa na Magufuli? tuko humu ndani sababu ya Magufuli na Samia walipita kila sehemu wakisema tupeni huyu tutafanya nae kazi, sababu yao watu wakachaguliwa”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents