Habari

M23 wadai mazungumzo ya amani DRC hayawahusu

Kundi la waasi wa M23 limesema jana kuwa halihusiki na tangazo la usitishwaji mapigano lililotolewa mjini Luanda, na kutoa wito wa mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Msemaji wa kisiasa wa kundi hilo Lawrence Kanyuka, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba M23 ameona waraka huo kwenye mitandao ya kijamii na hakukuwa na mwakilishi wao kwenye mkutano wa kilele wa Luanda, hivyo maazimio yake hayawahusu.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi na waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta walihudhuria mkutano huo mdogo wa kilele mjini Luanda siku ya Jumatano.

Mkutano huo uliwataka waasi kusitisha mapigano kufikia Ijumaa jioni, na kufuatiwa na kujiondoa kwenye maeneo yote yanayo kaliwa na M23 na kurejea kwenye maeneo yao ya awali.

Makubaliano hayo yamesema ikiwa watakataa kuondoka, kikosi cha Afrika Mashariki kinachopelekwa mjini Goma kitatumia nguvu dhidi yao.

Source DW

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents