Michezo

Mabadiliko makubwa Klabu Bingwa Afrika

Michuano ya Klabu Bingwa Afrika inaendelea na maajabu yake yanaendelea ni mara ya baada ya vilabu vilivyokuwa shirikisho msimu uliopita kufanya mabadiliko makubwa katika msimu huu kwa jailli ya Klabu Bingwa Afrika.

Timu hizo ni pamoja na Yanga SC, ASEC Mimosas, TP Mazembe hive vilabu vyote vimefanikiwa kufuzu kuelekea hatua ya robo fainali kwa kishindo;

Yanga mpaka sasa imekuwa ya pili kwenye msimamo wa kundi D huku kinara akiwa ni AL Ahly mwenye alama 9 wa tatu kwenye kundi hilo ni CR Belouizdad akiwa amejikusanyia alama 5 huku mshika mkia akiwa ni Medeama ya Ghana mwenye alama 4 tu huku wote wanasubiri michezo yao ya mwisho siku ya ijumaa ambayo itawakutanisha AL Ahly dhidi ya Yanga wakiwa wanapambania nafasi ya kwanza huku CR Belouizdad wakiwakaribisha Medeama ili kukamilisha ratiba ya michuano hiyo.

ASEC Mimosas baada ya sare na Simba huko nchini Ivory Coast na kujihakikishia kuwa na alama 11 na ndiye kinara wa kundi B huku Simba akiwa na Alama 6 baada ya huo mchezo.

Simba anajiandaa kumkaribisha Jwaneng Galaxy katika dimba la Benjamini Mkapa siku ya jumamosi Wekundu wa Msimbazi wanatakiwa kushinda mchezo huo ili kujihakikishia kuvuka na kwenda hatua ya robo fainali.

Wakati huohuo Wydad AC ya Morocco ikijiandaa kumenyana na ASEC Mimosas huku wababe Wydad wakitakiwa kuibuka na ushindi na kuombea Matokeo mabaya kwa Simba ili wao waweze kufuzu kuelekea robo fainali.

TP Mazembe wao tayari wamefuzu kuelekea hatua ya robo fainali na kipengele pese kilichobaki kwao ni nani atamaliza wa kwanza katika kundi A ikumbukwe kunguru wa Lubumbashi walishindwa kuvuka makundi katika michuano ya shirikisho Afrika na baada ya uwekezaji uliofanyika msimu huu wamejipata na sasa wamefuzu kuelekea robo akiwa na alama 10 kama kinara wa kundi akimuacha Mamelodi  Sundowns akiwa nafasi ya pili na alama 10 huku wakifuatiwa Nouadhibou ya Mauritania  wenye alama 4 huku Pyramid kutoka Misri akiwa na alama 4 pia.

Mchezo wa mwisho katika kundi hili ni katika ya Mamelodi Sundowns dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa huko South Afrika ili kutafuta timu itakayoongoza kundi A na wakati Pyramid watakuwa wanamenyana na Nouadhibou ya Mauritania mchezo huu utapigwa huko Misri ili kukamilisha ratiba ya hii michuano.

Kwa maana hiyo Vilabu vilivyoshiriki Kombe la Shirikisho msimu uliopita vinauwasha moto na kuzua gumzo balaa na hive vyote vilikuwa kwenye POT namba tatu vimefuzu kasoro AL Hilal ya Sudan ambayo mayo inasubiri mchezo wa mwisho ambao wataupiga dhidi ya Esperance De Tunis ya nchini Tunisia ili kuamua nani wa kufuzu hatua ya robo fainali.

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents