AfyaVideos

Maboresho makubwa yafanyika hospitali ya rufaa Tanga (+ Video)

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa we Tanga, ni kati ya hospitali kongwe zaidi kwani ujenzi wake ulianza mwaka 1896.

Pamoja na maboresho mengi yaliyofanyika katika hospitali hii mara kwa mara, zipo huduma muhimu zilizokuwa zikikosekana na kusababisha mateso makali kwa Watanzania waishio Tanga na maeneoo ya jirani pindi wanapihitaji huduma hizo. Moja ya huduma zilizokuwa zinakosekana ni kukosekana kwa huduma za kusafisha damu.

Lakini sasa, Serikali imejibu kilio cha muda mrefu cha watumiaji wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma hizo katika hospitali hiyo.

Awali, wagonjwa walikuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo jijini Dar es Salaam na kuweka maisha yao katika hatari zaidi au kuongeza gharama kubwa katika matibabu yao. Madaktari na wagonjwa, wameeleza furaha yao kufuatia uboreshaji huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents