Habari

Machinga Dar wakoshwa na kasi ya RC Makalla (Video)

Viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania SHIUMA wamefunga safari mpaka Mkoa wa Dar es salaam kumpongeza Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla kwa ushirikiano Mkubwa anaowapatia Machinga ikiwemo kuwasafirisha Viongozi wa Machinga na Bodaboda Nchini Rwanda kujifunza na uongozi rafiki kwa kundi la Machinga.

Miongoni mwa Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa Ndg.Matondo Masanja, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Viongozi wa SHIUMA Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kikao na Viongozi hao, RC Makalla amepokea maombi ya Viongozi wa SHIUMA Taifa ikiwemo Viongozi wa Taifa kupata fursa ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa Machinga Tanzania kufanyikia Dar es salaam.

Aidha RC Makalla Ameahidi kufanyia kazi ombi la Viongozi hao kukutana na Rais Dkt. Samia ambapo amesema atawasiliana na Mamlaka husika ili kufanikisha jambo Hilo.

Pamoja na hayo RC Makallaa ametoa wito kwa Viongozi wa SHIUMA Taifa kufanya kazi kwa pamoja na Viongozi wa SHIUMA Mkoa wa Dar es salaam Ili kwa pamoja waweze kuinua na kushughulikia changamoto za Machinga.

Hata hivyo RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Machinga kuendelea kufanya biashara kwenye Maeneo Rasmi* Ili waweze kunufaika na fursa za mikopo ambapo amesema Serikali Itaendelea kushughulikia changamoto zozote zitakazojitokeza.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents