Madagascar: Watu 46 wafariki katika makabiliano na wezi wa mifugo

Karibu watu 46 wamefariki nchini Madagascar katika makabiliano kati ya wezi wa mifogo na wanakijiji.

Shambulio hilo lilifanyika katika eneo la Marovitsika commune kusini – mashariki mwa nchi. Karibu wanaume 120 waliojihami kwa silaha walivamia vijiji viwili, Ambohitsohy na Vohitsimbe.

Tume ya kutetea haki za binadamu itafanya uchunguzi huru kubaini chanzo cha shambulio hilo. Inasema uchunguzi huo utasaidia kutoa usalama kwa wakazi.

Makabiliano kati ya wezi wa mifugo na wanavijiji hutokea mara kwa mara katika eneo hilo.

Related Articles

Back to top button