FahamuHabari

Madereva 17 wa magari ya IT wakamatwa Pwani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia madereva 17 wa magari yanayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi (IT) kwa kosa la kusafirisha abiria kinyume cha sheria ya usalama barabarani sura ya 168 inayokataza magari hayo kusafirisha abiria

Kwa mujibu wa Eatv.tv, Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo pamoja na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Edson Mwakihaba wamesema Magari hayo ya IT yanayoanzia safari  zao Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi za Zambia, Rwanda, Burundi na Congo kupita mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera yamekuwa yakisababisha ajali na kuleta madhara makubwa kwa abiria, hivyo hii ni operesheni endelevu ili kuzuia biashara hiyo hatarishi.

Wito wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani ni kuwataka abiria kutumia usafiri rasmi wa umma ili kuepusha usumbufu wanaoweza kuupata safarini kwa kukosa haki zao za msingi inapotokea ajali watumiapo magari ya IT.

Aidha amewataka madereva wanaoendelea kukaidi na kuvunja sheria ya usalama barabarani kwa makusudi kuacha mara moja kwani jeshi la polis litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents