Maelfu ya dozi bandia za Corona zakamatwa na Interpol

Polisi nchini China na Afrika Kusini wamekamata maelfu ya dozi bandia za chanjo ya Covid-19 na kuwakamata wahusika, Polisi wa kimataifa, Interpol wameeleza.

Ghala likiwa na dawa bandia za chanjo ya Covid-19

Polisi wamewakamata watu 80 kwenye kiwanda nchini China kwa madai ya kutengeneza chanjo bandia, ambapo dozi 3,000 zilibainika tayari zikiwa zimetengenezwa katika kiwanda hicho.

Raia watatu wa China na mmoja wa Zambia walikamatwa katika ghala huko Gauteng, Afrika Kusini, ambapo chupa zilizokuwa na dozi 2,400 ziligundulika.

Haijajulikana ni lini hasa watu hao walikamatwa. Kamatakamata nchini Afrika Kusini iliripotiwa na gazeti la Sunday Times mwishoni mwa mwezi Desemba.

Makablasha ya chanjo feki yalivyonaswa na polisi wa kimataifa

Siku ya Jumatato polisi wa Interpol walisema walikuwa wakipokea ripoti za kuwepo kwa mitandao ya kutengeneza dozi ghushi za chanjo ya Covid-19

Interpol (Shirikisho la Polisi wa Kimataifa) , lina makao yake jijini Lyon Ufaransa na husimamia ushirikiano wa kimataifa kati ya vikosi vya polisi na udhibiti wa uhalifu duniani.

Janga la virusi vya corona limegharimu maisha ya watu zaidi ya milioni 2.5 duniani kote na watu milioni 115 wameugua ugonjwa huo kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins.

Ikitangaza kuhusu kukamatwa kwa chanjo hizo feki, polisi wa Interpol wamesisitiza kuwa hakuna dawa ya chanjo iliyoidhinishwa ulimwenguni ambayo ”sasa inauzwa mtandaoni”.

”Chanjo yoyote inayotangazwa kwenye tovuti au kwenye mitandao ya biashara haramu, haitakuwa halali, ni dhahiri hazijafanyiwa majaribio na zinaweza kuwa hatari ,”. Ilisema taarifa ya polisi hao.

Polisi waligundua nini?

Huko Germiston, Gauteng, polisi walipata chupa zipatazo 400 – sawa na dozi 2,400 – za chanjo bandia na “idadi kubwa” ya barakoa bandia za 3M, Interpol ilisema.

Ilitoa picha za masanduku na vifurushi kwenye ghala.Makablasha ya chanjo feki yalivyonaswa na polisi wa kimataifa

Brigedia Vish Naidoo, msemaji wa jeshi la Afrika Kusini, amesema kuwa ushirikiano nan chi wanachama wa Interpol umedhihirisha kuwa na ”ufanisi sana”, wakati kukishuhudiwa ”ukamataji wa raia wa kigeni wakijaribu kuuza chanjo bandia kwa watu nchini Afrika Kusini”.

Afrika Kusini imeanza kutoa chanjo kwa raia wake tarehe 17 mwezi Februari baada ya kuwepo kwa wasiwasi kuhusu ufanisi wa chanjo dhidi ya kirusi kipya cha Covid-19.

Msemaji wa Wizara ya usalama wa Umma amesema polisi wanafanya kampeni maalum ya kuzuia na kukomesha uhalifu unaohusisha chanjo ya Covid” na kuwa wataendeleza ushirikiano na polisi wa nchi nyingine kuzuia uhalifu huo.

Tatizo ni kubwa kwa kiasi gani?

Katibu Mkuu wa Interpol Jürgen Stock amesema wakati operesheni za polisi nchini China na Afrika Kusini zikikaribishwa, hatua hii ni mwanzo tu likija suala la uhalifu unaohusiana na chanjo ya Covid-19.

Mwezi Desemba, Shirika hilo lilitahadharisha ulimwengu likionya polisi katika nchi wanachama wa ushirika huo kujiandaa kupambana na mitandao ya uhalifu inayolenga chanjo ya Covid-19 na kutoa ushauri kuhusu namna ya kugundua bidhaa bandia za kitabibu.

Mwezi uliopita, China ilimkata kiongozi wa mtandao wa uhalifu wa mamilioni ya dola uliokuwa ukitengeneza dawa ya Saline na maji ya kunywa ya chupa wakidanganya kuwa chanjo ya Covid-19.

Mshukiwa , aliyebainika kwa jina la Kong alifanya utafiti kuhusu mitindo mbalimbali ya vifungashio vya chanjo halisi kabla ya kutengeneza dozi zake 58,000. Alikuwa miongoni mwa watu 70 waliokamatwa kwa shutuma hizohizo.Huko Germiston, Gauteng, polisi walipata chupa zipatazo 400 - sawa na dozi 2,400 - za chanjo bandia

Kwa mujibu wa hukumu ya mahakama, Kong na timu yake walijipatia faida ya pauni milioni mbili kwa kuweka dawa ya kusafisha vidonda au maji ya kunywa kwenye mabomba ya sindano na kudanganya kuwa ni chanjo ya covid.

Bachi za dawa ghushi za chanjo zilisafirishwa kwenda ng’ambo lakini haikujulikana zilisafirishwa kwenda nchi gani.

Huko Mexico mwezi uliopita, polisi iliwakamata watu sita kwa madai ya kusafirisha chanjo bandia katika jimbo la mpaka wa kaskazini la Nuevo León.

Washukiwa walikuwa wamepanga kuuza chanjo kwa gharama ya dola za kimarekani 2,000 kwa kila dozi moja katika hospitali moja iliyo katika viunga vya Monterrey.

Related Articles

Back to top button