Habari

Maelfu ya Washia nchini wamuomboleza Iman Hussein

MAELFU ya Watanzania wameadhimisha kujitoa kwa Imam Hussein na wafuasi wake katika Vita vya Karbala ambapo maombolezo yamefanyika kwa siku kumi .

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandaliwa na Afisa Uhusiano wa Umma,
Kituo cha Utamaduni, Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Amani Salum ni kwamba tukio hilo la kila mwaka lilioandaliwa kwa siku kumi za maombolezo, lilihitimishwa kwa mikusanyiko mikubwa ya wafuasi wa Shia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na zaidi ya mipaka yake.

“Matukio haya yalikuwa na maandamano ya huzuni, hotuba za kusikitisha na kumbukumbu ya pamoja ya urithi wa kudumu wa Imam Hussein,”ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kwamba siku ya Jumanne, tarehe 16 Julai 2024, jumuiya ya Shia wa Tanzania waliandaa maandamano makubwa ya waombolezaji.

Alisema kundi la maombolezo liliandaliwa na Jumuiya ya Shia ya Khwaja Eznaashri, Dar es Salaam, na waombolezaji wengine kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, India, Pakistan, Lebanon, Iran na walishiriki.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Sheikh Noor Mohammad Rouhani, misionari kutoka Uingereza, alielezea lengo la Imam Hussein (AS) kama haki ya kijamii na kuasi kwake kama harakati ya kuhamasisha ambayo haikuzuiliwa na jiografia maalum.

“Nilijifunza kutoka kwa Hussein jinsi ya kupigana bila silaha. Nilishinda dhidi ya dhalimu anayeonekana kuwa na nguvu,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo ikinukuu maneno ya Sheikh Noor.

Akichangia Sheikh Al-Hadi Musa, Mkuu wa Jumuiya ya Amani na Usalama wa Kidini ya Tanzania (JMAT) alisema, yeye ni Sunni, lakini anaona ni jukumu lake kushiriki katika maadhimisho ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussain (AS).

Matukio ya maadhimisho yaliimarishwa zaidi na uwepo wa maafisa mbalimbali wa kisiasa na kidini, wakionyesha umuhimu wa urithi wa Imam Hussein katika nyanja tofauti za jamii.

Aliwataja miongoni mwa wahudhuriaji mashuhuri walikuwa ni wajumbe wa Bunge la Tanzania, Balozi Hussein Alvandi Behineh na Dk Mohsen Maarefi, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ilisema taarifa hiyo kwamba viongozi hawa, pamoja na wasomi na wawakilishi kutoka balozi jirani, walitoa msaada wao na kutambua tukio hilo, wakionyesha heshima na mapenzi ya ulimwengu kwa mchango wa Imam Hussein.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents