Habari

Mafuriko yaua zaidi ya watu 120 DRC

Takribani watu 120 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mafuriko ambayo yameukumba mji huo baada ya mvua kubwa kunyesha.

Vitongoji vya mji huo vimefurika na maji ya matope katika nyumba na barabara kuu katika mji huo wenye wakaazi milioni 15 zilifunikwa na maji.

Picha ambazo zinasambazwa mitandaoni zimeonesha maporomoko ya udongo katika wilaya ya Mont-Ngafula na kusababisa mpasuko kwenye barabara muhimu inayounganisha mji mkuu Kinshasa na bandari ya Matadi. Mnamo mwaka 2019, takriban watu 40 waliuawa kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents