Habari

Magamba ya samaki aina ya kaa kuzalisha nyuzi, tishu, nguo

MWANAFUNZI wa Shahada ya Uzamili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amebuni namna ambavyo magamba ya Samaki aina ya kaa yanavyoweza kuzalisha nyuzi ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya kushonea vidonda kwa wagonjwa na nguo.

Akizungumza na Bongo 5 katika banda la UDSM lililopo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Mhadhiri msaidizi chuoni hapo Cosmas Kindole amesema magamba hayo ya kaa yanapochanganywa na mwani ndipo yanaweza kutengeneza nyuzi hizo.

Amesema magamba hayo pia yakichanganywa na mwani yanaweza kutengeneza nguo za aina tofauti pamoja na karatasi nyeupe za kufutia mikono (tishu).

Kindiole amesema aliamua kuja na ubunifu huo baada ya kuona magamba ya Samaki hao yanazagaa mitaani hasa katika madampo ndipo akafikiria ni kwa namna gani ataweza kuzifanya taka hizo zirudi kwenye matumizi na kuleta tija kwa jamii.

“Magamba haya yanazalisha bidhaa ya nyuzi ambazo zinatumika kutengenezea nguona kushinea vidonda vya wagonjwa waliopo hospitalini, magamba haya yak aa yalikuwa ni uchafu unaotupwa ila sisi tumeweza kuutumia kwa kuurudisha katika matumizi kwa njia nyingine.

“Kwa mujibu wa takwimu tulizokuwa nazo mpaka sasa Afrika Masharikiinazalisha tani kati ya milioni sita had inane kwa mwaka za magamba haya ya samaki aina yak aa na yamekuwa yakitupwa kama uchafu,” amesema

Hata hivyo amesema mbali na magamba hayo ya Samaki, aina ya malighafi wanayoitafuta katika magamba hayo inaweza kupatikana kwa senene na ngisi na kwamba kupitia mwani na magamba hayo wamezalisha plastiki inayooza ambayo inawza kutumika kama vifungashio vya chakula.

Amesema gram 500 za magamba yak aa yanatosha kuzalisha kimiminika lita moja kilicho na uwezo wa kuzalisha nyuzi nyingi na ikiwa nyuzi hizo zitatumika kutengeneza nguo basi itakuwa fulana moja na jeans mbili.

Kindole amesema ubunifu huo ni sehemu ya kazi yake katika masomo ya shahada ya uzamili anayosoma na kwamba tayari wameshafanya majaribio ya nyuzi hizo katika kushona nguo ikiwa na ubora na kiwango kikubwa.
Aidha amesema utafiti wake huo upo katika hatua mbalimbali za kukamilisha na anaamini endapo utatumika ipasavyo utasaidia kupambana na uchafuzi wa mazingira na kuzalisha ajira.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents