Uncategorized

Magonjwa yasiyoambukiza yasabisha asilimia 40 ya vifo

Serikali imeeleza, takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakisababisha vifo kwa asilimia 40 katika maeneo baadhi nchini.

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Hargney Chitokolo

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Hargney Chitokolo wakati akifanya uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.

Ameeleza kuwa Magonjwa yasiyoambukiza duniani yamekua yakichangia vifo milioni 41 sawa na asilimia 71 huku nchini kwa sasa yakichangia kwa 40 katika baadhi ya maeneo nchini.

Hata hivyo amesisitiza kuwa hofu kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza yanawapata hwatoto wakiwa wadogo na kusababisha kuzorota kwa nguvu kazi.

“Nasema hivi mapema kwani unaweza kukuta sasa hivi watoto wadogo wana magoja ya sukari, presha na na kusababisha vifo vya chini ya miaka 60”. Chitokolo

Mbali na hayo, Mgeni rasmi amesisitiza kuwa Sekta ya afya pekee haitaweza kupambana katika janga hili kwa kuwa visababishi vingi vipo nje ya sekta ya afya na juhudi za pamoja ndizo zinazohitajika.

Juhudi za pamoja zilizobainishwa ni pamoja na kuboresha afya kwa kufanya mazoezi, kula mlo kamili, kubadili mtindo wa maisha kwa kuepuka tumbaku, vyakula vya mafuta, ulevi kupita kiasi. Huku wananchi wakishauriwa kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara.

Maadhimisho ya Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza yanaendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid ambapo yanafanyika Kitaifa Arusha  na kilele chake kinatarajiwa kuwa siku ya Ijumaa, Novemba 13.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents