HabariSiasa

Mahakama Burkina Faso yaamuru Compaore kulipa fidia kwa familia ya Thomas Sankara 

Mahakama nchini Burkina Faso Jummane imeamuru rais wa zamani Blaise Compaore na washtakiwa wengine tisa kulipa fidia ya zaidi ya dola milioni 1 kwa familia ya kiongozi wa zamani wa mapinduzi Thomas Sankara na washirika wake waliouawa mwaka wa 1987.

Uamuzi huo unajiri baada ya kesi ya mwezi uliopita ambayo ililihukumu kundi hilo la washtakiwa kifungo cha muda mrefu, na kumaliza kesi iliyoleta doa mbaya kwa taifa hilo la kanda ya Sahel kwa miaka 34.

Mshirika wa karibu wa Sankara , Compaore alichukua madaraka katika mapinduzi siku alipouawa Sankara, na kuongoza hadi 2014, wakati alipoondolewa madarakani kufuatia maandamano makubwa na kukimbilia ugenini.

Jaji Urbain Meda, aliyeongoza kesi katika mahakama ya kijeshi mjini Ougadougou, ameamuru malipo ya fidia ya dola milioni 1.3 kwa familia za watu 12 waliomaliziwa maisha wakiwa pamoja na Sankara.

Familia ya Sankara ilitunukiwa tuzo ya mfano.

Tuzo hiyo ni “ishara ya madhara ya maumivu na kiuchumi” yaliyoziathiri familia, Jaji Meda amesema.

Wanaotakiwa kulipa fidia hiyo ni Compaore, Hyacinthe Kafando, kamanda wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa Compaore, Gilbert Diendere, mkuu wa zamani wa jeshi mwaka wa 1987, na washtakiwa wengine 7.

Aprili 6, Compaore, Kafando na Diendere walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kupanga mauaji ya Sankara, huku wengine wakifungwa miaka mitatu hadi 20 jela.

Compaore, ambaye anaishi katika nchi jirani ya Ivory Coast, alihukumiwa bila kuwepo mahakamani, naye Kafando yuko mafichoni tangu mwaka wa 2016.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents