HabariSiasa

Mahakama ya Tanzania yaanzisha kituo cha kupokea taarifa

Mahakama ya Tanzania imeanzisha kituo cha kupokea taarifa kutoka kwa wadau wa Mahakama lengo likiwa ni kuboresha huduma ili ziendane na mahitaji yaliyopo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Elisante Ole Gabriel amesema kituo hicho cha kupokea taarifa kitakuwa msaada kwa wananchi pale ambapo watakuwa wamekwama kisheria na kuhitaji kupata ufafanuzi.

Ameongeza kuwa Pamoja na Mahakama kuwa sehemu sahihi ya kufanya maamuzi ya kisheria pia wapo watu wanaopindisha maamuzi hivyo kituo hiki kitakuwa msaada kwa wale watakaohisi kutotendewa haki

“Unajua Mahakama ni sehemu takatifu, hata mbinguni ni sehemu takatifu lakini si umeona kuna Ibilisi anachokoza chokoza, hivyo hata huku wapo watu wa aina hiyo, kwa hiyo kituo hiki kitakuwa msaada kupata ufumbuzi”- amesema Elisante Ole Gabriel

Ole Gabriel amesema kituo kisionekane kama kituo cha kukata rufaa badala yake ni kituo tu cha kupata ufumbuzi wa mambo ya kisheria kwenye mahakama.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents