Habari

Mahakama ya Uingereza yasema kumuita mtu kipara ni kosa

Mahakama nchini Uingereza imeamua kuwa ni kinyume cha sheria kwa wanaume kutukanwa baada ya mwanaume mmoja kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya muajiri wa kampuni aliyoifanyia kazi zamani.

Tony Finn, mwenye ummri wa miaka 64, alifanya kazi kwa miaka 24 kama fundi wa umeme katika eneo la West Yorkshire nchini Uingereza, kabla ya kufukuzwa kazi mwezi Mei, 2021.

Alidai kuwa Jamie King, mmoja wa wakurugenzi wakuu wa kampuni, alikuwa akimtusi kwa kuwa na upara, alipokuwa akielezea mzozo uliotokea mwaka 2019.

“Nilifunika vifaa kwa ajili ya kuvikarabati. Baada ya muda mfupi , niliona vifaa vikifunuliwa, na nikabaini kuwa Jamie King alikuwa amefanya hivyo . ” Aliiambia mahakama katika Finn.

Alisema kwamba kwasababu King alikuwa ni kijana mwenye nguvu, vitisho vyake vilisababisha hofu na hofu kwa maisha yake.

Jaji Jonathan Brain aliombwa kuamua kuhusu kosa la kumtusi mtu kwa kuwa na upara, na kulielezea kama “unyanyasaji wa kingono.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents