Mahindra na SARGA MotoCorp waungana kuboresha kilimo

Kampuni ya Mahindra & Mahindra Ltd. (M&M Ltd), kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza matrekta ulimwenguni kwa ujazo, leo imetangaza ushirikiano na kampuni ya SARGA MotoCorp ili kuimarisha biashara yake ya pembejeo za kilimo nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sarga Motocorp, Sandeep Singh (kushoto) na Meneja Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji Afrika na Kimataifa wa Mahindra, Sandresh Parab(kulia ) wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano kibiashara baina ya kampuni hizo mbili zenye lengo la kukuza sekta ya pembejeo za kilimo kwa kuuza na kutoa misaada sekta hiyo nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es salaam jana .
Pamoja na kuwepo nchini tangu 2008, kampuni ya Mahindra ina aina mbalimbali za matrekta na pembejeo zingine za kilimo, kwa mahitaji yote katika sekta nzima ya kilimo. SARGA MotoCorp, kampuni mashuhuri inayoendesha shughuli zake ulimwenguni kote, italeta utaalam wake wa Sekta ya Magari na ufahamu wake wa soko kwa lengo la kutoa uzoefu bora wa mauzo na baada ya mauzo kwa wakulima nchini Tanzania.
Kama sehemu ya ushirikiano kampuni ya Sarga MotoCorp imeanzisha uwanja wa maonyesho unaochukua takriban mita za mraba 300 kwenye Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, huku pia ikianzisha ghala la mita za mraba 800 na karakana katika eneo hilo hilo. Kama sehemu ya mpango mkubwa wa kupanua shughuli zake, kampuni ya Sarga MotoCorp pia inapanga kuongeza uwepo wake kote nchini kwa kufungua vyumba vya maonyesho sehemu nyingi zaidi katika miezi ijayo.
Kwa lengo la kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma ya kipekee. kampuni ya Sarga MotoCorp pia itachukua vituo vya kutolea huduma zaidi ya 25 vilivyoidhinishwa vya Mahindra (MCSP) na Wauzaji 3 wa Vipuri kote nchini Tanzania ili kuhakikisha upatikanaji wa vipuri vyenye ubora na huduma ya uhakika.
Akizungumzia kuhusu uzinduzi huo, Bw. Kedar Apte, Mkuu wa Uendeshaji wa Kimataifa – Sekta ya Pembejeo za Kilimo, kampuni ya Mahindra & Mahindra Ltd. alisema, “Tuna nia ya kubadilisha Kilimo na kuboresha Maisha ya wakulima duniani kote, Katika kampuni ya Mahindra tunajivunia kuendeleza madhumuni yetu kupitia Sarga MotoCorp nchini Tanzania. Kwa kuzingatia katika ubora katika sekta ya kilimo, kupitia ushirikiano huu hatutauza matrekta na vifaa vya kilimo pekee, bali tutaleta faida nyingi kwa mkulima wa Kitanzania kwa utendaji hali ya juu, tija, mapato na huduma rahisi baada ya mauzo. “
Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Bw. Sandeep Singh, Muasisi & Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya SARGA MotoCorp amesema, “Tunajivunia kutambulisha biashara yetu ya zana za shamba nchini Tanzania. Vile vile huu ni wakati wa fahari kwa SARGA MotoCorp kuweza kushirikiana na kampuni ya Mahindra ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza matrekta ulimwenguni.
Bw. Sandeep Singh aliongezea zaidi kwamba, “Mfumo huu vile vile utawapatia wateja huduma bora, kwa kuwepo kwa vito vya huduma zaidi ya 25 vilivyoidhinishwa. pamoja na wafanyakazi wenye mafunzo ya kutosha na uzoefu. Zaidi ya huduma bora, vile vile tutatoa waranti ya miaka miwili, na mwaka mmoja /masaa 1000 ya vifaa vya matengenezo vya mwaka 1/1000, ambavyo vinahakikisha utulivu kamili wa kiakili kwa wakulima wa Tanzania. Tumekusudia kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mipango kama vile “Jenga Kesho Iliyobora”, nchini Tanzania, ambayo inalenga kuimarisha ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo kwa maisha endelevu na yaliyoboreshwa”.
Kampuni ya Mahindra imekuwepo barani Afrika kupitia biashara yake ya matrekta na Magari kwa zaidi ya miongo miwili, ikisafirisha matrekta yake katika masoko zaidi ya 30 barani humu, ikiwa na uwepo mkubwa zaidi katika nchi za Tanzania, Algeria, Benin, Nigeria, Kenya, Sudan na Afrika ya Kusini. Katika magari, Mahindra ina bidhaa zinazohudumia mahitaji binafsi na kwaajili ya biashara, kama vile SUV na pick-ups, magari ya kati na mazito ya kibiashara, vifaa vya ujenzi na jenereta. Kampuni ya Mahindra kwa sasa iunafanya jitihada ya kuanza kutengeneza matrekta ya bei nafuu na vifaa vya kilimo na mitambo ya mazao kama vile mashine za kupandia mpunga, kuvuna mpunga, kuvuna nafaka na kupandia viazi, vilivyotengenezwa mahususi kwa ajili ya soko la Afrika.
Kuhusu Sekta ya Pembejeo za Kilimo za Mahindra
Mahindra ni nembo ya trekta nambari 1 ya India kwa zaidi ya miongo mitatu. Tangu kuzinduliwa kwa trekta ya kwanza mnamo mwaka 1963, kupitia ubia na kampuni ya International Harvester, Inc., USA, Katika mwaka 2019 kampuni ya Mahindra ikawa nembo ya kwanza ya trekta ya kihind kuuza matrekta milioni tatu ikijumuisha mauzo ya kimataifa.
Trekta za Mahindra, zinazojulikana kwa ubora na ufanisi wake wa kipekee kwenye ardhi tambarare na zile mbaya, zimeipatia kampuni hiyo Tuzo ya Deming na Medali za Ubora za Japani. Kampuni ya Mahindra ndiye watengenezaji pekee wa trekta waliofanikisha kufika hatua hii. na leo hii, ina moja ya aina mbalimbali za matrekta zilizotengenezwa kwa matumizi ya kazi mbalimbali kwa soko la ndani na la kimataifa.
Leo, Mahindra ipo katika zaidi ya nchi 50 katika mabara sita, huku Amerika ikiwa ndio soko kubwa zaidi nje ya India. Kampuni pia ina vituo vya inatengeneza na kuunganisha matrekta vilivyopo sehemu mbalimbali ulimwenguni, na ikiwa na shughuli zake katika nchi za Amerika Kaskazini, Brazili, Mexico, Ufini, Uturuki, na Japan kupitia kampuni tanzu.
Kuhusu Mahindra
Kundi la la makampuni la Mahindra lilianzishwa mwaka wa 1945, ni mojawapo ya shirikisho kubwa zaidi la kimataifa la makampuni yenye wafanyakazi 260,000 katika zaidi ya nchi 100. Inaongoza katika utengenezaji wa pembejeo za kilimo, magari ya matumizi, teknolojia ya habari na huduma za kifedha nchini India na ni kampuni kubwa zaidi ya trekta duniani kwa kiasi. Ina uwepo mkubwa katika nishati mbadala, kilimo, usafirishaji, ukarimu na ujenzi. Kundi la Mahindra lina lengo la wazi la kuongoza ESG duniani kote, kuwezesha ustawi wa vijijini na kuimarisha maisha ya mijini, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya jamii na wadau ili kuwawezesha kukua kiuchumi.