Burudani

Maisha ya Ndoa na Muziki; Kwa Shilole wembe ni ule ule

Msanii wa Bongo Flava, Shilole amema si kweli kuolewa kwake kunamfanya kushuka kimuziki.

Muimbaji huyo akizungumza katika show ya Davido mwishoni mwa wekeend iliyopita amesema kuwa amekuwa kimya kutokana ana kazi nyingi nje ya muziki ila sio ndoa.

“Sio kweli, mimi ningekuwa nimepungua kwenye game usingenifanyia interview sasa hivi. Sio kweli nina kazi nyingi za kuniingizia fedha kuliko muziki,” alisema Shilole.

Tangu Shilole aipoolewa December 06, 2017 hajatoa wimbo wowote, wimbo wake wa mwisho kutoa unaitwa Kigori ambao ulitoka August 07, 2017.

Licha ya Shilole kuwa msanii kwa upande mwingine ni mjasiriamali ambapo kwa sasa anamiliki biashara kadhaa kama mgahawa wa chakula ‘Shishi Food’, na bidhaa za Shishichili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents